top of page

Zisikizeni Nyimbo

Zisikizeni nyimbo(tamu) toka Bethlehemu, leo kazaliwa Masihi wetu Yesu, sauti hizo nzuri (sana) ni za malaika wanaotangaza kuzaliwa kwa Yesu x2

1. Ee Yesu mpendwa utujaze roho, na pendo lako, mwisho tufikie, ufalme wa mbingu, Bwana turehemu sisi wenye dhambi, twakulilia, kwa mapenzi yako tufike kwa Baba.


2. Ee Mwana wa Maria, Yesu kipenzi, Karibu kwetu, utulishe roho na Umungu wako, ili roho zetu zikujue wewe, Rabi mwema, yote utakayo, tuyatende Bwana.


3. Utukufu wako, wauwacha juu, Mungu kitoto, nasi kwa imani, twakukaribisha, umekuja kwetu kwa unyenyekevu, Rabi mwema, Karibu rohoni, Emmanueli Yesu.

4 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page