top of page

Yesu Mimi Ninakutamani


Yesu mimi nimekutamani, kuungana nawe Yesu wangu , nionje tena pendo lako, ili niwe na faraja tele x2, (ninaomba (ooh) ee Bwana wangu, uniokoe mawimbi yamezidi, uje unisaidie) x2

1. Ninaomba neema zako, ili nivuke salama Bwana, niuone uzuri wako niwe na amani tele. 2. Hofu nyingi kila mahali, bila wewe Yesu nitashindwa, ndiwe mwamba niwe salama, katika maisha yangu.

3. Maadui nishambulia pande zote waniangamize, njoo Bwana unioke mikonono mwa adui zangu. 4. Wewe ndiwe mwangaza wangu, niongoze nifike salama, niinue kutoka chini na kunipandisha juu.

5. Wewe ndiwe wangu mfariji, njoo Bwana tuliza mawimbi, unibebe nibembeleze, Mungu Baba tulizo langu.

0 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page