top of page

Yesu Nakushukuru


Yesu nakushukuru, (asante) x4 { Umenilisha, asante, umeninywesha, asante, Umenipenda, asante, umenilinda, asante) x2

  1. Ee Bwana wangu nitakushukuruje, Kwa pendo lako lisilo na kipimo, Unanipenda Bwana nasema asante, Bwana,

  2. Umenitunza kwa msingi wa kweli, Naburudika kwa wingi wa divai, Unanipenda Bwana nasema asante, Bwana,

  3. Kwa pendo lako wanilinda salama, Kwa wema wako ninapata fanaka, Unanipenda Bwana nasema asante, Bwana,

  4. Ee Yesu wangu nitakushukuruje, Kwa ukombozi na zawadi ya mbingu, Unanipenda Bwana nasema asante, Bwana,

1 view0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page