top of page

Yesu Mwokozi Wangu

Yesu Mwokozi wangu, karibu rohoni mwangu ninakukaribisha x2

Mwili wako Yesu chakula cha uzima, damu yako Yesu kinywaji cha uzima wewe ni Mwokozi wa roho yangu x2

1. Njoo Bwana , shibisha roho yangu kwa mwili wako, tuliza kiu yangu kwa damu yako.

2. Njoo Bwana, uishi ndani yangu na mimi kwako, ili niushiriki umungu wako.

3. Njoo Bwana, nipe nguvu za mwili wangu dhaifu, usiokidhi haja ya roho yangu.

4. Njoo Bwana, tawala roho yangu ee Mungu wangu, na unilinde dhidi ya ibilisi

5. Njoo Bwana, uwe kiongozi wangu wa maisha, na mwisho nishiriki ufalme wako

2 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page