top of page

Yesu Kristu Atawala

Yesu Kristu atawala milele yote Yesu Kristu ndiye Bwana wa mabwana wote Yesu Kristu atawala milele yote Yesu Kristu ni mfalme wa wafalme wote


Yeye ndiye Mwana wa Mungu aliyetukomboa kwa damu yake Mataifa njooni tumwimbie Tumfanyie shangwe Mungu wetu Tuzitangaze rehema zake, pia na utukufu wake Ili mataifa yote duniani Yapate kumjua Bwana Nao wote waliopotea, waweze kumrudia Mungu


Alikuja duniani, kwa ajili yao, ili mi niliye mdhambi nipate kuokolewa Alipata mateso mengi kwa ajili yangu mimi


Tazama uwezo wake, Mwana wa Mungu Limfufua Lazaro kutoka katikati ya wafuTazama na yule kipofu, alimponya akapona


Alifanya miujiza mingi duniani Alitoa pepo wachafu, aliponya na wagonjwaAliyakemea mawimbi, bahari ikawa shwari


Njoo sasa ndugu yangu, kwake Bwana Yesu Tatizo lako lolote ulilo nalo litakwisha Njoo ufanyiwe maombi kwa Yesu yote yawezekana

9 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page