top of page

Yesu Aliniita Njoo

Yesu aliniita, ‘Njoo, Raha iko kwangu,

Kichwa chako ukilaze kituani mwangu.‘

Nilikwenda kwake mara, Sana nilichoka;

Nikapata kwake raha na furaha.


Yesu aliniita, ‘Njoo, Kwangu kuna maki:

Maji ya Uzima, bure, unywe uwe hai.‘

Nilikwenda kwake mara na maji nikanywa:

Naishi kwake na kiu kamwe sina tena.


Yesu aliniita, ‘Njoo, Dunia i giza,

Ukinitazama, nuru `takungarizia.‘

Nilikwenda kwake mara, Yeye jua langu,

Ni kila wakati mwanga safarini mwangu.

6 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page