top of page

UTUKUFU

SOL: Utukufu kwa Mungu juu

Na amani duniani yote.

ALL: Kwa watu wenye mapenzi (mema) x 2

1. Twakusifu twakuheshimu, twakuabudu, twakutukuza,

All: Mungu wa majeshi ewe Baba x 2

2. Twakushukuru Mfalme, wa mbingu Mungu Baba yetu

All: Mungu wa majeshi ewe Baba x 2

3. Ufutaye dhambi zetu tuhurumie tusikilize

All: Mungu wa majeshi ewe Baba x 2

4. Uketiye kuume kwa Baba, upekee yako Yesu kristu

All: Mungu wa majeshi ewe Baba x 2

5. Naye roho mtakatifu, katika utukufu wa Baba

All: Mungu wa majeshi ewe Baba x 2

NASADIKI

Nasadiki kwa Mungu mmoja Nasadiki x 2

Mimi kweli nasadiki mimi - Nasadiki x 2

Ndiye Baba mwenyezi Nasadiki x 2

Mwumba mbingu na dunia - Nasadiki x 2

Na kwake Yesu kristu Nasadiki x 2

Nasadiki kwa Mungu mmoja Nasadiki x 2

1. Mwanaye wa pekee

Atokaye kwa baba

Kazaliwa na Bikira

Kwa roho mtakatifu.

2. Kisha akasulubiwa

Kwa amri ya pilato

Akafa na kazikwa

Kashukia kuzimu

3. Yeye akafufuka

Kapaa juu mbinguni

Kaketi kuume kwake

Mungu Baba mwenyezi

4. Tarudi kuhukumu

Wazima pia wafu.

Kwa roho mtakatifu

Kanisa katoliki

5. Shirika takatifu

‘Ndoleo la dhambi zetu

Nangojea ‘fufuko

Uzima wa milele.


MTAKATIFU

Mtakatifu Bwana – Ee Mungu wa majeshi x 2

Mbingu na dunia – Ee zimejaa utukufu x 2

Hosana – juu mbinguni x 2

Hosana juu mbinguni.

Mbarikiwa yeye – Ajaye kwa jina la Bwana x 4


FUMBO LA IMANI

Kristu alikufa

Kristu alifufuka

Kristu atakuja – atakuja tena x 2


AMINA

Amina A – amina – Amina A – amina x 2

Amina – A – amina x 2

Amina – A – amina x 2


BABA YETU

Baba yetu uliye juu mbinguni - Baba

Jina lako Ee Baba nalo nalitukuzwe - Baba

Ufalme wako nao ufike Baba

Utakalo Ee Baba kweli nalifanyike - Baba


Baba yetu Baba x 3 ) x 2

Duniani Ee Baba kama Mbinguni - Baba

Tupe leo mkate wetu wa kila siku - Baba


Tusamehe Ee Baba makosa yetu - Baba

Kama vile twasamehe waliotukosea - Baba


Situtie Ee Baba majaribuni - Baba

Walakini Ee Baba utuopoe - Baba

Maovuni Ee Baba utuopoe - Baba

Maovuni Ee Baba kweli utuopoe - Baba


Kwa kuwa ufalme ni wako Baba - Baba

Na nguvu vyoteni vyako - Baba

Utukufu Ee Baba hata milele - Baba

Utukufu Ee baba kweli hata milele - Baba

5 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page