top of page

Wimbo wa Historia

Wimbo huu uliimbwa historia watu wote mnaombwa msikize kwa makini ilikua october hamsini na mbili watu wote tulisikia kenyatta ameshikwa hakushikwa kenyatta pekee yake lakini

alishikwa na mabingwa wa uhuru Wooi wooi woooooi

ilikua kilio nchini kenya watu wote tuliona huzuni mwingi sana

wakina baba akina mama na watoto wote walilia machozi wakisema


Woooi woooooi wooi tunataka kenyatta aachiliwe

baba wa taifa alipotoka gerezani aliwakuta wajumbe wetu wametengana vibaya sana aliongoza wajumbe mpaka ulaya

kufika huko alipigwa na mayai yaliyooza mzee wetu hakujali alishinda na kurudi na katiba ya nchi yetu hapa kenya

mzee wetu alituomba tusahau yaliyopita badala yake tuijenge nchi yetu ooh asante baba wetu wengi wee asante baba wetu

13 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page