top of page

Wewe ni Mungu


Sikia aa sikia Bwana, Sikia aa sikia Bwana sauti yangu Sikia aa sikia leo Sikia aa sikia Bwana sauti yangu.


Hii sauti inabeba hisia zangu Zilizomo moyoni mwangu sikia Bwana sauti yangu Naeleza furaha niliyo nayo Na hamu ya kukushukuru sikia Bwana sauti yangu. Nakufunulia moyo wangu uko wazi, Nakumiminia, sifa na tenzi Mwenyezi, Napiga kelele usikie Bwana sauti yangu Sikia aa sikia Bwana ( Mungu we) Sikia aa sikia Bwana sauti ya moyo, Moyo,moyo, wangu moyo, moyo, moyo ha ha- Nimejua ya kwamba - wewe ni Mungu kila wakati Naona wazi kwamba - wewe ni Mungu kila wakati Kwenye furaha - wewe ni Mungu kila wakati Na kwenye magumu bado- wewe ni Mungu kila wakati Haupungui neno - wewe ni Mungu kila wakatii

  1. Hukutaka raha zinipe kiburi - aeee eee ukanipimia. Na taabu ziliponishambulia - ukafungua (Bwana) mlango nikatoka salama.

  2. Na vipaji ona hukunipa vyote - aaee eee ukanipimia. Ingawaje nilipoweka juhudi - ukafungua( Bwana) mlango nikatoka salama.

  3. Sikuumbwa msafi kama ulivyo - aaee eee ukanipimia. Hata hivyo dhambi iliponisonga - ukafungua ( Bwana) mlango nikatoka salama. Yeyeyeye yeyeyeyeye yeyeyeyeyeeeeee Nakuja nimebeba sifa kukuzungushia Maana utukufu ni wako milele na milele- Nakuja nimebeba sifa kukuzungushia Maana utukufu ni wako milele na milele. Nakuja nimebeba shangwe, na chereko Nakuja nimebeba kinanda watu wakuimbie- Nakuja nimebeba sifa kukuzungushia Maana utukufu ni wako milele na milele. Nakuja nimebeba sifa kukupamba nakuja nimebeba maua jama watu wakutukuze- Nakuja nimebeba sifa kukuzungushia Maana utukufu ni wako milele na milele. Milele na milele, milele na milele, milele na milele,milele ni Mungu wa pekee... x5 (Bass) Wewe ni Mungu, wewe ni Bwana, we ni mwema, utabaki Mungu X2 * ( Tenor) wewe ni wa kwanza ni Mungu weee, wewe ni wa mwisho eee Unaitwa Alfa ni Mungu wee, wewe ni Omega eee

Milele ni Mungu wa Pekee

7 views0 comments

Commentaires

Noté 0 étoile sur 5.
Pas encore de note

Ajouter une note
bottom of page