top of page

Watumishi wake Baba



1. Watumishi wake Baba wangapi waliopo, Wanakula na kusaza chakula chake Baba

Nami - Nami nataabika hapa (Nashi) Nashiriki na nguruwe (Chaku) Chakula kisichofaa, yanipasa kurudi (Nita) Nitarudi na kusema (Baba) Baba yangu nisamehe (Nime) Nimekosa kwake Mungu, na mbele yako Baba

2. Baba kamwona yu mbali kashikwa na huruma, Akakimbia kumlaki kamkumbata na busu

3. Baba sistahili tena kuitwa mwana wako, Unifanye kama mmoja wa watumishi wako

4. Baba yangu nimekosa ninaomba huruma, Unisamehe nirudi nikakutumikie

5. Bwana karibisha mimi kwenye karamu yako, Meza imeandaliwa inaningoja mimi

6. Nasongea ninakuja ninakukimbilia, Mimi ni mtoto mpotevu Baba unipokee

7. Nimekula nimeshiba nakushukuru Baba, Chakula kama asali asante sana Baba


15 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page