top of page

Watu Wote

Watu wote waimba, Halleluiah Hosanna

Yesu amezaliwa, Mwokozi wa dunia,

Mwokozi wa yatima, Mwokozi wamataifa,

Mwokozi wa wajane, Mwokozi wa wagonjwa

- Hosanna halleluiah, halleluiah hosanna


Mwimbieni Bwana, Halleluiah Hosanna

Kelele za shangwe, wakina baba waimba,

wakina mama waimba, watoto wote

waimba, vijana wote waimba,

Yesu amefufuka - Hosanna halleluiah,

Halleluiah hosanna


Enyi watu wote, mpigieni Mungu kelele za

shangwe, pigeni makofi, pigeni kinanda

nyimbo za furaha, nyimbo za zaburi

- Hosanna halleluiah, Halleluiah hosanna


Heri walio maskini, heri wenye huzuni

heri wenye upole, heri wenye njaa, heri

wenye rehema, heri wenye moyo safi,

heri wenye kiu- Hosana Halleluiah, Halleluiah Hosanna


Sisi sote twaimba, Yesu ni Bwana Mwumba

wa dunia, Mwumba wa mbinguni, Mfalme

wa amani, Mfalme wa upendo,

Mfalme wa furaha

- Hosanna Halleluiah, Halleluiah hosanna.


Yesu ni Bwana, Yesu ni Mungu, Yesu ni

Mfalme, Yesu ni Baba, Yesu ni rafiki Yesu

ni mponyaji, Yesu ni Mkombozi - Hosanna

Halleluiah, Halleluiah hosanna.


Mungu Baba Halleluiah Halleluiah

Hosanna, Mungu Mwana Halleluia

Mungu Roho Halleluia, Mungu Moja

Halleluia, Halleluiah Hosana,

1 view0 comments

Commentaires

Noté 0 étoile sur 5.
Pas encore de note

Ajouter une note
bottom of page