top of page

Wakupeleka Hukumuni


Wakupeleka hukumuni Yesu, ili uamuliwe na mtu Tendo gani umefanya Yesu, hata wakutaka sulibiwe Ulikuja kwangu, mi mdhambi Ili uniokoe katika taabu zangu zote Unipatanishe na Mungu aba ili nifike kwake kwenye uzima wa milele Kwa nini unateseka hivyo, Bwana usiye na kosa lolote Mimi ndiye mwenye kosa Yesu, Nawe ndiwe wa kunihukumu Msalaba mzito waubeba Mijeredi kupigwa, taji la miiba kuvalishwa Yote umekubali, juu yangu Ili unikomboe, mimi mdhambi wa huzuni (Nimekosa mimi nimekosa unihurumie Mungu wangu) x2

  1. Mpumbavu amesema moyoni hakuna Mungu Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza Toka mbinguni Mungu aliwachungulia wanadamu Aone kama yupo mtu mwenye akili amtafutaye Mungu

  2. Ee Mungu kwa jina lako uniokoe Na kwa uweza wako unifanyie hukumu, Ee Mungu uyasikie maombi yangu Uyasikilize maneno ya kinywa changu.

0 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page