top of page

Simameni Tucheze


  1. Wakristu wote simameni, simameni Tuchezeni mbele za Bwana, kwa shukrani (Leo) Asubuhi na mchana nitamsifu (Bwana) Na usiku nitaita jina la Bwana (wangu) Sifa zake zi kinywani mwangu daima nitaimba sifa zake Mungu milele

  2. Tupeperusheni mikono juu hewani Tushangilieni tupigeni makofi

  3. Ametulisha kwa chakula cha mbinguni Twaburudika kwa kinywaji cha uzima

  4. Ametukinga na maovu ya dunia Mapenzi yake kwetu sisi ni ya ajabu

  5. Turukeruke na tucheze kama ndama Tupigeni ngoma kayamba na vinanda

5 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page