top of page

Waimbaji wa Mungu

Mwimbieni Bwana wimbo ule mpya maana ametenda mambo ya ajabu.Paazeni sauti imbeni saburi tangazeni sifa zake Mungu wetu x2

  1. Waimbaji wa Mungu- imbeni kwa shangwe, chezeni kwa furaha mbele zake Bwana. Pigeni tarumbeta -vinanda na zeze, ngoma na baragumu hata na kayamba (wote)

  2. Mpeni bwana Mungu -enyi watu wake, mpeni utukufu mpeni na nguvu. Mwabuduni daima -kwa uzuri wake iteni jina lake kwa utakatifu (wote)

  3. Sauti yake bwana -i juu ya maji, na tena ina nguvu inayo adhama.Yawalisha ayala -sauti ya Bwana, na wote wanasema utukufu wake (wote)

  4. Yeye hufanya jua- liwake mchana, nao mwezi na nyota usiku wa giza. Anawalisha ndege- wote wa angani, na wote wana sema utukufu wake (wote)

  5. Mungu ni wa upendo- amejaa huruma, rehema zake kweli hazina mpaka. Fadhili zake Bwana -zinadumu kweli, milele na milele hata na milele (wote)

4 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page