top of page

Uzuri wa Yesu


(Kwa imani yangu, matendo na maneno, Nihubiri neno la Mungu siku zote, nipeleke neno la Mungu pande zote, Mataifa wanangojea neno hilo) x2

  1. Kwa ajili yake Yesu Kristu Bwana wangu, Kwa ajili ya uzuri wake wa daima uzuri wake Yesu usio na kiasi, Nitende yote mema nifanane na Yesu.

  2. Kwa ajili yake Yesu Kristu Bwana wangu, Nimeyasahau maneno ya zamani ya kale yamepita shetani ameshindwa, Nimempata Yesu natembea na yeye

  3. Kwa ajili yake Yesu Kristu Bwana wangu, Kwa ajili ya uzuri wake wa daima, nakaza mwendo sana nipeleke ujumbe, Ujumbe wake Yesu kwa mataifa yote

  4. Kwa imani pia matendo na maneno, Kwa upendo pia upole na kiasi, Nimeweka msingi imara kwake Yesu, Usiotikisika daima siku zote

7 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page