top of page

Uzuri wa Kifo

Basi ndugu zangu, hatimaye imetosha Acheni kunung'unika kuhusu kifo Jitayarisheni ili mfe kifo chema Hiyo hekima ya kweli na ucha Mungu kamili Kifo ni zawadi ya upendo toka kwa Mungu Nacho kimeandaliwa kuivuka dunia chungu Ibada na dini zenu ni upuuzi mtupu Kama mwisho wake siyo kumfikia Mungu Lakini hamuwezi kumfikia Mungu Isipokuwa kwa njia hii ya kifo

  1. Dhambi ya Adamu ilimfanya Adamu, akajificha mbali na uso wa Mungu Akapewa kifo, kusudi roho yake irudi karibu na Mungu milele

  2. Kifo kilibeba maana yake halisi, alipoinuliwa Mwokozi wa watu Akashinda kifo, kusudi watu wake baada ya kifo warudi kwa Mungu

  3. Kama hampendi, taabu za ulimwengu, kwa nini mwaogopa kujitayarisha Kupokea kifo, kusudi muiage dunia mpokee raha ya milele

  4. Tofautisheni, kifo nayo mauti, mauti humpeleka mwenzetu kuzimu Ingawaje kifo, humtenganisha mwenzetu na taabu za dunia hii

3 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page