top of page

Utamu wa Yesu


1. Ndugu zangu nawauliza mbona mnashangaa kuniona ninavyoimba pia kuchezacheza, mimi sijachanganyikiwa wala sijapagawa basi mtegeni sikio leo niwaeleze


Mimi nimeonja utamu ule wa Yesu (utamu). Ni mwili na damu utamu ule wa Yesu (utamu) basi ninaimba utamu ule wa Yesu, ninanesanesa utamu ule wa Yesu, pia ninadunda utamu (ule wa Yesu utamu)

2. Mwili wake amenilisha damu yake ameninywesha, ameniahidi uzima, uzima wa milele. Dhambi zangu ameziosha sasa mimi msafi, pendo lake nimelionja kweli ninatangaza


3. Na magonjwa ameniponya mimi ninayo afya, kwa hakika amenikinga nazo hatari zote. Bwana amejaa huruma, huruma na neema wala yeye hana hasira ni mwingi wa fadhili


4. Onjeni muone ya kwamba Bwana wetu yu mwema, elekezene macho juu na mtatiwa nuru. Mtafuteni Bwana Mungu angali yu karibu, naye Bwana atayajibu maombi yenu yote


5. Bwana ni mchungaji wangu sitaogopa kitu, katika majani mabichi yeye ananilaza. Na katika njia za haki yeye huniongoza, ananijalia chakula changu cha kila siku

7 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page