top of page

Usipange Foleni



Usipange foleni kwenye duka la shetani, Utauziwa dhambi faida yake mauti Nenda ukajipange dukani kwa Bwana Yesu, Utapata kibali cha kuingia mbinguni

  1. Enyi wavuta bangi, na madawa ya kulevya Mbona mmejipanga katika duka la shetani

  2. Na ninyi wala rushwa, makahaba na wachawi Mbona mmejipanga katika duka la shetani

  3. Duka lake shetani limejaa vitu vingi Tena vyapendeza sana na kuuvutia moyo

  4. Ramani ya mbinguni nenda kwake Yesu Ramani ya kuzimu shetani ndiye mchoraji

  5. Mnaofunga ndoa katika jinsia moja Nanyi mmejipanga katika duka la shetani

  6. Mavazi ya aibu dada zetu mwajivika Mnaita vimini shetani anachekelea

6 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page