top of page

Usiniulize

1. Usiniulize kwa nini ninafuraha, ninashangilia moyoni nina amani, tulizo ya kweli rohoni wacha niseme, sababu ya haya jamani mnisikize

Nimepata (nafasi) ya kushiriki (karamu) imeandaliwa na Yesu mwenyewe katika altare, na sasa mimi (nashukuru) kwa ukarimu (wake Bwana) kutuandalia karamu takatifu katika altare

2. Usiniulize kwa nini mimi naimba, nimeburudika moyoni nina upendo. Nguvu zake Bwana kwa kweli yamenijaza, maana ya haya wenzangu nita tangaza.

3. Usinulize kwa nini na metameta, tabasamu nyingi usoni nimejaliwa. Maringo ninayo hakika nina uzima, tegeni sikio nikawaeleze kwa nini.

4. Usiniulize kwa nini narukaruka, napiga makofi vifijo vigelegele. Mwendo wa madaha kwa kwelii nitazikwenda, sasa inabidi niseme sababu gani.

1 view0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page