top of page

Usia wa Maria



Sisi wana wa dunia tukumbuke maneno aliyosema Bikira Maria, Alipo watokea watoto wa Fatima, Lucia, Francisi na Yasinta, (Alisema tusali, tusali Rozari tupate a-amani, natuwaombee wale wakosefu wasio na mwombezi, na wasiomwamini Yesu Mwokozi wamuamini ili waokoke) x2


Mama yetu anahuzunishwa sana na matendo yetu maovu anajua adhabu yetu ijayo hivyo anaona huruma sa-ana.


Atusihi tuache dhambi kwa dhati kumkosea Yesu tuyatubu makosa yetu yote ili Bwana atupatie amani


Tusitende tena maovu na dhambi atusihi mama wa Yesu Tusimkasirishe tena Mungu asije tutupa motoni milele.


Ibada ya moyo safi wa Maria tuizingatie daima Tuipokee komunyo takatifu kila jumamosi ya kwanza ya mwezi.

7 views0 comments

Commentaires

Noté 0 étoile sur 5.
Pas encore de note

Ajouter une note
bottom of page