top of page

Upendo na Ukarimu

  1. Watu wengi tunajaribu upendo Tunawajali wale wanaotuhusu Tunaojua wataweza kutulipaHatuwathamini wale wasiotuhusu wala wasiojiweza, lakini

  2. Tunawakopesha wenye kipato kikubwa Tukiamini nao watatukopesha Wakitujia wenye shida na fukara Tunawakimbia eti hawakopesheki Na wana madeni mengi, lakini

  3. Wakiugua wenye nafasi za juu Tunajazana kwao na vichupachupa Tukiamini na sisi tukiuguaWatalundikana kwetu na vifuko fuko Kadi na michango mingi, lakini

  4. Tukitembelewa na mtu mwenye viraka Tunauliza kama tulimualika Akija aliyeshuka kwenye shangingi Tunamwuliza kinywaji anachokunywa Tena kwa unyenyekevu lakini

5 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page