top of page

Uniondolee Dhambi


Uniondolee dhambi, nitakase, Unioshe niwe mweupe pe x2

1. Nakiri makosa yangu, naziona dhambi zangu, Unioshe niwe mweupe pe.


2. Mimi kweli mkosefu, tangu kuzaliwa kwangu, Mwenye dhambi tangu tumboni mwa mama yangu


3. Hivyo unafanya vyema, wewe unaponihukumu, Una haki unaponiadhibu


4. Wewe wataka unyofu, ule unyofu wa ndani, Nifundishe hekima moyoni


5. Niumbie moyo safi, na uweke ndani yangu, Roho mpya iliyo thabiti.

13 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page