top of page

Unaposimama

1. Unaposimama kwenda mbele zake Bwana, Hiyo ni ishara kwamba u pamoja naye, (Bali kama ndugu yangu unafanya hivyo, Kwa kujionyesha ni heri hata usitoe, Ukifanya hivyo ndugu unajipa laana) x2


Sadaka ya moyo nakutolea Baba wa milele pokea sadaka ya moyo wangu na uibariki.


2. Hebu fikiria sasa ni baraka ngapi? Umeshazipata tangu tumboni mwa mama, (Kisha ukifika hapa kutoa sadaka, bado moyo wako ndugu unanung’unika, unakushauri keti utatoa kesho) x2


3. Neno lake Bwana pia linatuamuru, tumtolee yeye sala na mapato yetu, (kisha ukitoa sala na mapato yako, usijiulize hizi zitaenda wapi, jua watangaza neno lake Bwana Mungu) x2


4. Siku nyingi Bwana mimi nimejitolea, kukutumikia kwa vipawa mbalimbali,(lakini kunavyo pia vipawa vingine, unionyeshapo mimi ninavifunika, nikidhani kwamba hayo ni mambo ya kale) x2

7 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page