top of page


  1. Nasikia sauti nzuri, kama ya malaika, Ni sauti toka mbinguni, sauti ya Mungu, Aniita mimi niende nikamtumikie, Anitume shambani mwake, nikavune yote.

  2. Ninaenda mimi naenda, ninaenda mwenyewe, Ninaenda mbele za Bwana, sitarudi nyuma Ndugu zangu na marafiki mniache niende, Nikafanye kazi ya Bwana, nitakapotumwa.

  3. Nilitazama moyo wako, moyo wako mwanangu, Hata kabla hujazaliwa nilikutambua, nilikuteua mapema, kati ya ndugu zako, Uwe kuhani wangu mimi, kuhani mkuu.

  4. Shamba lake Bwana ni kubwa, na mavuno ni mengi, Wavunaji ndio wachache, nitakwenda mimi. Twakuomba sana ee Bwana, tupeleke shambani, Tukavune mavuno yote, yaliyo tayari.

  5. Uwe nami siku kwa siku, Bwana usiniache, Unikinge na majaribu, nilinde daima, nipeleke habari njema, ulimwenguni mwote, Watu wote wakutambue, wakugeukie.

3 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page