top of page

Umekosa Nini

  1. Tuifuate Njia ya Msalaba, tuifuate mpaka Kalvari Tusimamapo bila haya, (msalaba *2) huponya roho

  2. Umekosa Nini we Yesu, kushtakiwa bure kwa Pilato Wenye kustahili hukumu, si wewe, si wewe, Bwana ni sisi

  3. Ole msalaba huo mzito, apagazwa Mwana Mpenzi wa Mungu Mwili waenea mateso, alipa, alipa madhambi yetu

  4. Ona Mumba Mbingu na nchi, yupo chini mzigo wamwelemea Na mtu kiumbe chake kwa ukali, ampiga, ampiga bila huruma

  5. Huko njiani we Maria, waonaje hali ya mwanao Ni damu tupu na vidonda, machozi, machozi yamfumba macho

  6. Kwa Simoni heri ya kweli, mimi pia Yesu nisaidie Kuchukua mzigo wa ukombozi, kuteswa, kuteswa pamoja nawe

  7. Uso wa Yesu malaika, Bethlehemu wakuabudu Bahati yake Veronika, kupangusa, kupangusa mfalme wa mbingu

  8. Wakimvuta huku na huku, wauaji wakamchokesha bure Chini wamtupa bado kwa nguvu, aibu, aibu yao milele

  9. Wanawake wa Israeli, msilie kwa sababu hiyo Muwalilie hao kwa dhambi, upanga, upanga ni juu yao

  10. Mwokozi sasa ni ya tatu, kuanguka chini ya msalaba Katika dhambi za ulegevu, nijue, nijue kutubu hima

  11. Muje malaika wa Mbingu, funikeni mwiliwe kwa huruma Vidonda vyake na utupu, askari, askari wamvulia

  12. Hapo mkristu ushike moyo, Bwana wako alazwa msalabani Mara miguu na mikono, yafungwa, yafungwa kwa misumari

  13. Yesu mpenzi nakuabudu, msalabani unapohangaika Nchi yatetemeka kwa hofu, na jua, na jua linafifia

  14. Mama Maria mtakatifu, upokee maiti ya mwanao Tumemwua kwa dhambi zetu, twatubu, twatubu kwake na kwako

  15. Pamoja naye kaburini, zika dhambi na ubaya wa moyo Yesu tuwe wakristu wa kweli, twakupa, twakupa sasa mapendo

  16. Katika roho yangu Bwana, chora mateso niliyokutesa Nisiyasahau madeni, na kazi, na kazi ya kuokoa

2 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page