top of page

Tunakuja kwako Baba na maombi yetu (Baba) utusikilize Baba utuhurumie. Tazama watu – wanavyo kufa kila siku. Ugonjwa wa ukimwi unatumaliza. Ukimwi haujali lugha, ukimwi haujali taifa, ukimwi haujali rangi x2 Wazee, vijana, watoto, hao wote wanakufa

Ulimwengu wote unajiuliza juu ya ugonjwa huu, unaomaliza watu katika dunia hii, waganga wanajitahidi hawajapata madawa. (Mungu tusaidie tunakulilia x2


Ukitembelea familia nyingi katika nchi yetu, utawakuta watoto wasio na wazazi, wajane wameongezeka, hawapati msaada Mungu x2


Watu wengi bado hawajakubali kwamba ukimwi upo, lakini wafundishwa juu ya ugonjwa huu, wameshindwa kujihadhari, na ugonjwa wa ukimwi (ukimwi ni hatari watu kufa wote x2


Watu wote ondokeni tupigane na ugonjwa wa ukimwi, silaha yetu ni Mungu anayetuongoza, tufundishe wenzetu wote ili wajihadhari. (Sote tujihadhari, na ugonjwa huu x2

0 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page