top of page

Ukarimu wa Bwana



1. Nani kati ya watawala wote wa wafalme wa dunia hii, aliye wahi kuandaa karamu akawaalika watu wote?

Ni nani kama Bwana Yesu Mfalme wa mbingu na nchi anayetualika sote kwa karamu aliyoiandaa bali tuwe na moyo safi x2.

2. Sote tunaalikwa kushiriki kwenye karamu yake Bwana, tukiwa tajiri au maskini bali tuwe na moyo safi.

3. Ishara ya mapendo makubwa kwetu kutoka kwake Bwana Yesu, kutoa mwili kutoa damu yake kuzishibisha roho zetu

4. Ni fundisho kutoka kwake Bwana tuonyeshe ukarimu, kwa ndugu rafiki hata majirani daima maishani mwetu.

5. Enyi wafalme watawala wote mliojaliwa kwa mali, toeni sehemu za hazina yenu saidieni maskini.

31 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page