top of page

Twendeni wote kwa Bwana (TB I 8-6)

Twendeni wote kwa Bwana, atualika karamuni,

Tukale mkate wa mbingu.

  1. Yeye mwenyewe ni Mungu,Na pia ni mwanadamu, jamani.

  2. Yeye ni mkate halisi,Yeye ni shibe halali, jamani.

  3. Yeye ni Mwana wa Mungu,Mtawala Mkuu wa mbingu, Jamani.

  4. Yeye ni penzi la Baba,yeye ni Neno la Baba jamani.

  5. Yeye ni mwanga wa kweli,Tena ni njia ya kweli, jamani.

  6. Yeye ni mpenzi wa wote,faraja kweli kwa wote, jamani.

  7. Yeye ni mlango wa mbingu,Tuzo na heri ya mbingu, jamani.

4 views0 comments

Commenti

Valutazione 0 stelle su 5.
Non ci sono ancora valutazioni

Aggiungi una valutazione
bottom of page