top of page

Twendeni kwa Karamu

1. (Karibuni kwa karamu) – Asema Yesu Mwana wake Mungu, (tubuni mjitakase), twendeni kwa karamu yake Bwana x 2

Twendeni – Twende kwa karamu

Tukale – mwili wake Bwana

Tukanywe – Damu takatifu

Tupate – kujaliwa mema

Twende – Twendeni

Twende – Twendeni, twende, twende

(Twende kwa karamu, twende kwake Bwana x 2)

2. (Atakaye nipokea)- asema Yesu Mwanga wa dunia, (uzima ataupata) – ataishi milele na milele x 2

3. (Chochote tunachotenda) – cha hitaji mwangaza wake Yesu, (pasipo wake mwangaza) – maisha yetu hayana msingi

4. (Yeyote aniombae) – asema Yesu Mkombozi wetu, (nitamwombea kwa Baba) – ili ahadi yangu itimizwe x 2

18 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page