top of page

Twende Sote Waumini

Bass: Twende sote waumini tupeleke zawadi Wote: Kwake Baba Mungu wetu B/T: Tulivyo navyo vyote ni vyake tupeleke Wote: Kwake Baba Mungu wetu S/A:Mkate tunaleta, divai tunaleta S/T: Kazi ya mikono yetu Wote: Twakusihi Baba pokea S/A: Mazao tunaleta na fedha tunaleta, S/T: Japo ni kidogo sana Wote: Twakusihi Baba pokea.

  1. Mkate huu uwe mfano wa mwili wako Baba pokea, Divai hii iwe ishara ya damu yako Baba pokea (twaomba)

  2. Mavuno yetu ni jasho letu, sisi wanao, Baba pokea, shukrani zetu na shida zetu, twakutolea Baba pokea (twaomba)

  3. Mawazo yetu, na nia zetu twakutolea Baba pokea, furaha yetu, uchungu wetu, twakutolea Baba pokea (twaomba)

  4. Maombi yetu, twakutolea, sisi wanao Baba pokea, matendo yetu, mateso yetu, twakutolea, Baba pokea (twaomba)

  5. Na nyoyo zetu, twakutolea tunakuomba Baba pokea, na vyote Baba, tunavileta, uvibariki uvipokee (twaomba).

15 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page