top of page

Twakuomba Mama Maria

  1. Mama Maria Mwombezi wetu, mama wa neema na hu-ruma Tusikilize Mama wa Yesu, tusikilize wakosefu Twakuomba Mama Maria, kwa Mwanao Mama tuombee Sala zetu Mama Maria, kwa Mwanao mama zifikishe Nyoyo zetu Mama Maria, zatamani kufika mbinguni

  2. Mama Maria uliye mwema, tuliza nyoyo zetu wanao Tunaposhindwa tusaidie, tusije baki katika giza

  3. Mama Maria twakuamini, mama wa Mungu msaada wetu Matumaini yetu ni kwako, katika shida tusimamie

  4. Mama Maria usituache, umpelekee Bwana maombi Atubariki wenye mashaka, tupate uzima wa milele

2 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page