top of page

Tushukie Masiya

Tushukie, Masiya, kutuokoa dhambini, Mkombozi ee, Masiya, njoo, njoo, njoo.

  1. Tumekosa, tumeacha, kumpenda Mungu mwenyezi kwa dhambi zetu nyingi. Twakulilia wewe, uje kutupatanisha. Twakutamani sana, njoo, njoo,njoo

  2. Sisi watu, nivipofu, hatuoni njia zake Mungu dunyani kwetu. Twakulilia wewe, uje uwe mwanga wetu. Twakutamani sana, njoo, njoo, njoo.

  3. Udhaifu, wetu mkuu, tunashindwa kutimiza amri zote za Mungu. Twakulilia wewe, uje kutuimarisha.Twakutamani sana, njoo, njoo,njoo.

  4. Ufahamu, wetu mdogo, hatujui kupendana hatumwelewi Baba. Twakulilia wewe utufundishe hekima. Twakutamani sana, njoo, njoo,njoo.

  5. Tunakosa, kiongozi, ili atutangulie tuweze kumfuata. Twakulilia wewe, upate kutuongoza.Twakutamani sana, njoo, njoo,njoo.

2 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page