top of page

Tushangilie Yesu Amezaliwa


Basi tushangilie shangwe shangwe shangwe tupigeni makofi shangwe shangwe shangwe kwani humu mna nini, ni mwana wa Mungu aliyezaliwa x2 shangilia

  1. Yesu amezaliwa aie mjini kule Bethlehemu x2 twendeni tumpokeni masiha wetu na mkombo zi wetu ni na zawadi tumtunuku yule aliyezaliwa x2 Shangwe

  2. Na wale wachungaji aie mjini wametangulia x2 kwenda kushuhudia mkombozi wetu alikozaliwa, nasi tu mashahidi wa Habari njema tulizoletewa x2 Shangwe

  3. Malaika mbinguni aie hosanna wanamuimbia x2 wanamuinamia mtoto mchanga aliyezaliwa, wanamsujudia Emanueli Mungu Pamoja nasi x2 Shangwe

  4. Tumpe na zawadi aie zawadi zinazo pendeza x2 kwa ngoma na kayamba twendeni wote tukamshangilie, Yesu mwana wa Mungu azaliwe ndani ya mioyo yetu x2 Shangwe

33 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page