top of page

Tumesisimuka


Tumesisimka (kweli) tunakuja kwako ee Baba, Tumeandama (sote) tunaleta zawadi zetu, waumini wote simameni twende pamoja, tupeleke fedha mavuno na mifugo yetu } *2

  1. Ondokeni Baba na mama ondokeni nanyi watoto Chukueni fedha na mali, tupeleke mbele za Bwana (Tuweke akiba mbinguni, nasi tutabarikiwa) x2

  2. Hima hima twende pamoja, hima hima twende kwa Bwana Tupeleke furaha zetu, tupeleke uchungu wetu (Simameni twende kwa Bwana tupeleke nyoyo zetu) x2

  3. Fedha za mifukoni mwetu tupeleke kwa ukarimu Na mapato ya nguvu zetu, tupeleke kama zawadi (Twende kwake tumshukuru, sote tupate Baraka) x2

  4. Mavuno tuliyojaliwa, kutokana na jasho letu Mifugo tunaowafuga, tupeleke kama sadaka (Tutabarikiwa zaidi, Bwana atatubariki) x2

  5. Mkate mazao ya ngano, divai tunda la zabibu, Kageuza mwili na damu, tutakula na kubakisha, (Tutapata nguvu zaidi, na uzima wa milele) x2

6 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page