top of page

Tumeingia Kwako Bwana

Unison)Tumeingia kwako Bwana, tunaimba kwa furaha nyumbani mwako. x2 Tuko mbele zako asubuhi tumekuja

Nyumbani mwako Mungu Baba utupokee utubariki x2


  1. Kwa shangwe kubwa vigelegele na nyimbo Baba tumekuja-hekaluni mwako. kwa vinanda kwa vinubi kwa machezo Baba tumekuja –hekaluni mwako.

  2. Bwana ututakase sisi wanao leo asubuhi-Altareni mwako, Bwana utujalie baraka zako leo asubuhi- Altareni mwako.

  3. Nyumba yako ni nyumba ya sala tumekuja tupokee-utusikilize. Dua zetu maombi yetu na sala zetu zipokee-utusikilize.

  4. Nyua zake Bwana kweli zapendeza macho njooni nyote-njooni tumwabudu, ingieni malangoni mwake kwa furaha tumwabudu- leo na milele.

27 views0 comments

תגובות

דירוג של 0 מתוך 5 כוכבים
אין עדיין דירוגים

הוספת דירוג
bottom of page