top of page

Tumaini Langu


  1. Mungu Muumbaji wa mbingu na dunia, wewe muanzilishi wa maisha yangu, waniongoza kwenye milima hata mabonde, wewe kiongozi mwema (Bwa-na) nakuamini Bwana

  2. Changamoto nyingi zinazoniandamana, nakutegemea uwe faraja kwangu, kwako nitapata heri na neema yakutosha, hujapungukiwa kitu (Bwa-na) nakuamini Bwana

  3. Usafiri wangu kazi ya mwanadamu, nakutegemea uwe dereva wangu, barabarani angani hata kwenye bahara, mwelekezi wangu mkuu (Bwa-na) nakuamini Bwana


Watu wote mliovunjika mioyo (vunjika mioyo), ninyi nyote mnaokata (tamaa msichoke) tamaa leo kumbukeni Mungu wenu,mtafuteni siku zote, kumbukeni kiongozi wenu mwenyezi Mungu, Mayatima na wajane njooni kwake (njooni njooni kwake), wote mlio wanyonge karibieni leo (karibieni leo), kumbukeni Mungu wenu,mtafuteni siku zote, kumbukeni kiongozi wenu mwenyezi Mungu, Yeye tumaini tumaini letu tumaini tumaini Mungu atuajali tumaini letu, Tuseme tumaini tumaini letu tumaini tumaini Baba atupenda tumaini letu, Tuimbe tumaini tumaini letu tumaini tumaini Mungu atukinga tumaini letu.

1 view0 comments

Comentários

Avaliado com 0 de 5 estrelas.
Ainda sem avaliações

Adicione uma avaliação
bottom of page