top of page

Tulishangilie Neno



1. Simameni tulipokee neon hili la uzima limetushukia kutoka juu mbinguni.Ni neno lenye Wokovu ni neno lenye ushindi watu wote tulishike tukombolewe

Neno lake Bwana Munguni neno lililo jema ni neno lililo hai latuongoza Neno lake Bwana Mungu ni taa yatumulika ni nuru yatuangaza twametameta. Tulishangilie (neno) tulifurahie (neno) tupige vigelegele sote tumepata neon (neno)

2. Tuandamaneni pamoja tukisifu na kuimbamikononi tumelibeba neno la MunguKwa furaha na machezo kwa vifijo na nderemo neema ya Mungu imetujia kwa neno

3. Baba soma somo la kwanza mama soma somo la pili watoto waimbe zaburi na aleluya, Kasisi soma Injili Askofu ahubiri waumini tegeni sikio msikie.

4. Mataifa na makabila viongozi na watawala lisomeni neon ili mpate fahamu Someni agano la kale torati na zaburi tubuni tubuni na kuamini injili.

5. Vitu vyote ulimwenguni vinakuja vitapita lakini neno la Mungu ladumu milele Hapo mwanzo lilikuwapo bado liko na litakuwa neno lake Mungu litasimama daima

27 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page