top of page

Tujongee Mezani

Tujongee mezani mwake Bwana, tukampokee Mwokozi wetu. (Akae daima pamoja nasi, atujaze neema rohoni mwetu. tupate uzima wa milele x 2.)

  1. Yesu mwenyewe anatualika, kwa karamu ya uzima wa roho. Twende mbele yake tukampokee, Mwokozi mwema na mnyofu wa moyo.

  2. Njooni waumini twende tukampokee, watu wote wenye njaa kweli. Rohoni mwetu tumkaribishe, aishi daima pamoja nasi.

  3. Ni upendo wake Yesu mwenyewe, kujitoa mwili na damu yake. Twendeni wote tukashiriki, kina baba kina mama na vijana.

  4. Yeyote yule mwenye njaa na kiu, chakula kipo mezani mwa Bwana. Kushibisha roho zetu sisi sote, tuwe na Yesu pamoja milele.

  5. Kina mama baba na vijana, tushangilie Bwana kwa wokovu. Na tuna sema asante hakaika, kwa zawadi aliyo tupatia

1 view0 comments

コメント

5つ星のうち0と評価されています。
まだ評価がありません

評価を追加
bottom of page