top of page

Tiririsha- Baraka Top-Top


  1. Asante kwa kila jambo latoka kwako liwe baya, liwe zuri nakushukuru (unaleta mvua, kwa watu wote, mwanga wako unatumulikia wote wema na wabaya) x2 (Tiririsha Bwana baraka za mbinguni zote, tiririsha Bwana kwa watu duniani kote) x2 (tujazie mpaka zijae top top, tiririsha baraka na neema top top tushushie mpaka zimwagike kote tulipo) x2

  2. Jambo baya twaomba Bwana lipite mbali kwa mapenzi na wema wako tutashukuru (kwani wewe Bwana muweza yote umetuumba kwa mkono wako kwa mfano wako) x2

  3. Ziwafikie baraka zako na wagonjwa kule mawodini neema ya utakaso wako na upako wako uwafike, Kwa walio ofisini washushie nako top top kwa walio majumbani washushie nako top top, kwa walio mitaani washushie nako top top kwa walio safarini washushie nako top top. (Teremsha tupokee wanao tulio hapa) x2


306 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page