top of page

Tazameni uwinguni


Yesu - ni Bwana wa mabwana, Ni Mungu wa miunguMfalme Yesu, ni mfalme milele x2

  1. Tazameni uwinguni, tazameni Mbinguni kwa Baba Anakuja mtawala anakuja Bwana wa majeshi Anakuja na hukumu zake na ujira wake mikononi Anakuja duniani kote atawale mataifa

  2. Tazameni uwinguni, tazameni mbinguni kwa Baba Anakuja mhubiri anakuja mtabiri wetu Anakuja na maneno yote ya kitabu chake mkononi Anakuja ayasome yote yatokaye kwake Mungu

  3. Tazameni uwinguni, tazameni mbinguni kwa Baba Anakuja daktari anakuja mwenye kutuponya Anakuja mwenye matibabu na madawa yake mikononi Anakuja awatibu wote wagonjwa wapate afya

1 view0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page