top of page

Tazameni Miujiza ya Mungu

Tazameni miujiza ya Mungu, tazameni maajabu, anayotutendea, viumbe tuishio duniani katuumba sura mfano wake, mwili wenye kupendeza, akili ya maarifa yenye utashi wa kila namna nafikiri mimi ninafikiri, Bwana ni nani ni nani ni nani, ni nani, ni nani, aliye sawa na wewe Muumba Tumpigie makofi, shangwe, watu wote, leo ni shangwe, ufukweni mwa bahari, tuimbe wote tumtukuze Mungu x2


Nafikiri nafikiri, mimi nimeumbwa vipi, Maajabu yake Mungu, kaniumba mi nilivyo


Dunia ilivyoumbwa, ni kweli Inashangaza, yenye wanyama mimea na ardhi yenye rutuba


Nashukuru ee Mungu, kwa mema uliyonipa, milele hata milele, utukuzwe Mungu wangu

5 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page