top of page

Tazameni Meza ya Bwana


Tazameni meza ya Bwana (kweli) inapendeza (kama nini), Bwana Yesu ameandaa (leo)karamu kubwa (kweli kweli) Ni chakula chenye uzima chakula cha roho x2.

  1. Bwana alivyo mkarimu kautoa mwili wake, kaitoa kama chakula cha wokovu wetu.

  2. Mwili wa Bwana ni chakula bora cha uzima, damu yake Bwana ni kinywaji cha kweli.

  3. Bwana ametualika sote tujongee mezani, tukale chakula cha uzima wa nyoyo zetu.

  4. Simama ndugu nenda mbele kwa chakula cha uzima, ni chakula chenye uzima chakula cha roho.

9 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page