top of page

Taita Mass

Bwana Bwana Utuhurumie -

Bwana, Bwana Utuhurumie

Ee Bwana Ee!

Ee Bwana Ee!

Ee Bwana Utuhurumie


Kristu, Kristu utuhurumie -

Kristu, Kristu utuhurumie

Ee Kristu Ee!

Ee Kristu Ee!

Ee Kristu Utuhurumie


Bwana, Bwana….


UTUKUFU

‘Tukufu! ‘Tukukufu kwa Mungu Juu

Amani! Na amani duniani

(Kwa watu wenye mapenzi - wenye mapenzi mema) x2


A-ma-ni!


Sifa! Sisi tunakusifu

Heshima! Sisi tunakuheshimu

(Tunakuabudu - Sisi tunakuabudu) x2

He-shi-ma!


‘Tukufu! Sisi tunakutukuza

Shukrani Sisi tunakushukuru

Kwa ‘jili ya utukufu - Utukufu wako mkuu x2

Shu-kra-ni!


Ee Mungu! Ee Bwana Mungu

Ee Baba Mfalme wa mbinguni.

Ee Mungu Baba - Mungu Baba Mwenyezi x2

Ee Ba-ba!


Ee Bwana! Ee Bwana Yesu Kristu

Ee Mwana Kristu Mwana wa pekee

Mwana wa Baba - Mwanakondoo wa Mungu x2


Ee Mwa-na!

Mwokozi Mwenye kuondoa dhambi.

Huruma! Dhambi za dunia

Utuhurumie - Pokea ombi letu x2


Hu-ru-ma!

Ee Yesu Kwani ndiwe Mtakatifu

Ee Kristu Kwani ndiwe Bwana.

Ee Yesu Kristu - Ndiwe peke yako Mkuu! x2


Ee Kri-stu!

Umoja! Pamoja na Roho Mtakatifu.

Milele! Katika utukufu,

‘Tukufu wa Mungu Baba - Kristu anaishi x3


Mi-le-le


NASADIKI

Nasadiki kwa Mungu mmoja x2

Mwumba mbingu na dunia x2

Na kwa Bwana Yesu Kristu

Mwana wake wa pekee


Nasadiki kwa Mungu Baba -

Nasadiki nasadiki Mungu aliyetuumba

nasadiki nasadiki

Na kwa mwana mkombozi -

Na kwa roho wa uzima -


Alitungwa kwa uwezo wake x2

Roho mtakatifu x2

Kazaliwa na Maria

Yule mama na bikira


Akateswa kwa Pilato ndipo x2

Akasulibiwa x2

Kafa tena akazikwa

Akashuka kuzimu


Siku ya tatu kafufuka, akapaa x2

Hata mbinguni x2

Amekaa kuume kwa Mungu

Baba aliye Mwenyezi


Atakuja kuhukumu wazima pia x2

Na wafu x2

Na ufalme utakuwa

falme wake wa milele


Nasadiki kwa kanisa takatifu x2

Takatifu Katoliki Katoliki

Shirika la watakatifu

Maondoleo ya dhambi zetu


Nangojea ufufuko wa miili x2

Toka kwa wafu x2

Na uzima wa milele

Yote hayo nasadiki


MTAKATIFU

Mtakatifu Bwana Mungu wetu -

Ee Hosana juu!

Mtakatifu Bwana Mungu wetu -

Ee Hosana juu!

Mtakatifu Bwana Mungu wetu -


Ee Hosana juu!

Mbinguni - Mbinguni

Utukuzwe Bwana Mungu - Ee!

Mungu Muumba wetu - Ee!


Mbingu na dunia zimejaa - Ee! Ee! Ee!

Utukufu wako - Ee!

Ee, Ee, mbinguni - Ee,Hosana juu

mbinguni


Utukuzwe Bwana Mungu - Ee!

Mungu Mkombozi wetu - Ee!

Uliangamiza mauti ukaleta - Ee! Ee! Ee!

Uzima mpya - Ee!

Ee, Ee, mbinguni - Ee, Hosana juu mbinguni


Utukuzwe Bwana Mungu - Ee!

Mungu mfariji wetu - Ee!

Ulimtuma Roho kwetu tuwe - Ee! Ee! Ee!

Sote mwili mmoja - Ee!

Ee, Ee, mbinguni - Ee, Hosana juu mbinguni


FUMBO LA IMANI

Kristu, Kristu, Ee! - Kristu alikufa,

Kristu, Kristu, Ee! - Kristu alikufa,

Kristu! Ee Kristu, Kristu! - atakuja tena Kristu.


BABA YETU

Baba yetu uliye mbinguni

Baba yetu, Baba yetu

jina lako litukuzwe daima

Ee Baba, Ee Baba, Ee!


Baba yetu uliye mbinguni jina lako

litukuzwe daima

Ufalme wako ufike, utakalo lifanyike

duniani kama mbinguni


Baba yetu -

utupe leo mkate wetu wa kila siku,

utusamehe makosa yetu, kama

tunavyowasamehe na sisi waliotukosea

usitutie katika kishawishi lakini utuopoe maovuni


Kwani ufalme ni wako - Baba yetu

Kwani nguvu ni zako - Baba yetu

Utukufu ni wako - Baba yetu

Baba, milele, milele - hizi zote zako,

Baba!


MWANA KONDOO

Mwana Mwana kondoo wa Mungu

Uondoaye Uondoaye

Dhambi za dunia - Dhambi za dunia

Utuhurumie utuhurumie


Utujalie amani Utujalie amani

14 views0 comments

Comentarios

Obtuvo 0 de 5 estrellas.
Aún no hay calificaciones

Agrega una calificación
bottom of page