top of page

Subukia Mass



Bwana, Bwana Bwana utuhurumie x2

Kristu utuhurumie, Kristu utuhurumie x2

Bwana, Bwana Bwana utuhurumie x2


UTUKUFU JUU KWA MUNGU

Utukufu juu kwa Mungu, na amani dunianai, kwao watu wenye mapenzi, watu wenye mapenzi mema x2

1A: S/B: Tunakusifu tunakuheshimu, twakuabudu tunakutuza. 1B: A/T: Twakushukuru kwa ajili yako, ya utukufu wako mkuu.

2. S/B: Ee Mungu Baba ndiwe Mfalme wa mbinguni Baba Mwenyezi A/T: Ee Yesu Krisru Mwana wa pekee, Mwana Kondoo Mwana wa Baba.

3. S/B: Uondoaye dhambi za watu, tuhurumie, tusikilize. A/T: Tuhurumie mwenye rehema, maombi yetu uyapokee.

4. S/B: Uketiye kuume kwake Mungu Baba tuhurumie. A/T: Kwa kuwa ndiwe pekee yako, pekee yako Mtakatifu.

5. S/B: Pamoja naye Roho Mtakatifu, katika utukufu wake A/T: Anayeishi na kutawala milele yote Amina.


MTAKATIFU

Mtakatisu, Mtakatifu, Mtakatifu Mungu wa majeshi. Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.


Hosanna, hosanna, hosanna, hosanna juu mbinguni.


Mbarikiwa anayekuja kwa jina la Bwana.


MWANAKONDOO

Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia utuhurumie x2

Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia utujalie Amani.



68 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page