top of page

St. Veronica Mass

Ee Bwana (Bwana Mungu) utuhurumie (ee Bwana) ee Bwana Mungu (tuhurumie) utuhurumie (ee Bwana ee Mungu Mungu utuhurumie

Ee Yesu (Kristu) utuhurumie Ee Yesu Kristu utuhurumie


UTUKUFU

  1. Utukufu (juu) kwa Mungu Mbinguni Na amani iwe kote duniani (tunakuabudu) Tunakusifu Bwana twakuheshimu Bwana tunakuabudu Twakutukuza Bwana twakuheshimu Bwana

  2. Ewe Bwana Mungu Baba mfalme wa Mbinguni Tunakushukuru kwa utukufu mkuu, Mungu Baba Mwenyezi

  3. Ewe Bwana Yesu Kristu Mwana wa pekee Mwana kondoo Mungu uondoaye dhambi, utuhurumi-e

  4. Uondoaye dhambi zetu utusikie, Ewe uketiye kuume kwa Mungu Baba, utuhurumi-e

  5. U pekee Bwana Mtakatifu na u Kristu Pamoja naye Roho katika utukufu, wake Mungu milele

ALELUYA

Aleluya (aleluya) aleluya (aleluya) aleluya aleluya

NASADIKI

  1. Nasadiki (kwa Mungu Baba), nasadiki (kwa Mungu Mwana) Nasadiki (kwa Mungu Roho) nasadiki

  2. Nasadiki kwa Mungu mmoja Baba ye-tu Mwenye-zi Nasadiki Yesu Kristu mwana wake wa pekee Nasadiki alipata mwili kwa Roho Mtakati-fu Nasadiki kazaliwa na Bikira Maria

  3. Aliteswa alisulubiwa kwa amri ya Pnsyo Pilato Akafa na akazikwa na kushuka kwa wafu Alifufuka siku ya tatu na kupaa juu Mbingu-ni Toka huko tarudi kuhukumu ulimwengu

  4. Nasadiki kwa Roho Mtakatifu na Kanisa Katoliki Nasadiki Ushirika wao Watakatifu Nasadiki ufufuko wa miili na ondoleo la dhambi Nasadiki uzima wa milele na milele

MTAKATIFU

  • Mtakatifu (Bwana Mungu) Mtakatifu (wa Majeshi) *2 Mbingu na dunia zimejaa zimejaa Zimejaa utukufu wako Bwana

  • {Hosanna juu Mbinguni Hosanna Mbinguni juu Hosanna juu } *2 Amebarikiwa amebarikiwa yeye Yeye ajaye kwa jina lake Bwana

FUMBO LA IMANI

  • Yesu Kristu alikufa Yesu alifufuka Atarudi Yesu atakuja tena

AMINA

  • Amina (amina) amina (amina) amina amina

BABA YETU

  1. Baba Yetu uliye Mbinguni, jina lako litukuzwe daima Na ufalme wako na ufike na mapenzi yako yatimilike Utakalo (utakalo) lifanyike (lifanyike) duniani (duniani) kama Mbinguni *2

  2. Tupe leo na mkate wetu tupe mkate wetu wa kila siku Tusamehe na makosa yetu vile tusameheavyo wengine

  3. Situtie vishawishini bali utuopoe maovuni Situtie vishawishini bali utuopoe maovuni

  4. Kwa maana ufalme ni wako na nguvu pia nao utukufu Kwa maana ufalme ni wako na nguvu pia nao utukufu

MWANA KONDOO WA MUNGU

  1. Ee Mwana Kondoo wa Mungu, Unayeziondoa dhambi za dunia (dhambi zote za dunia) Tuhurumie (tuhurumie) utuhurumie

  2. Ee Mwana Kondoo wa Mungu, Unayeziondoa dhambi za dunia (dhambi zote za dunia) Tuhurumie (tuhurumie) utuhurumie

  3. Ee Mwana Kondoo wa Mungu, Unayeziondoa dhambi za dunia (dhambi zote za dunia) Tupe amani (tupe amani) utupe amani

3 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page