top of page

St. Stephen Mass


Ewe Bwana ‘tuhurumie (wote) [Ewe Bwana ‘tuhurumie Kwani sisi tuwakosefu (ewe) x 2] x 2

Ewe Kristu ‘tuhurumie

Ewe Bwana ‘tuhurumie


UTUKUFU

Utukufu kwa Mungu mbinguni, na amani kwa watu wema.


Twakusifu tunakuheshimu, twakuabudu tunakutukuza x 2


Utukufu kwa Mungu juu na amani, kwa watu wema pote duniani.


Tunakushukuru m-falme wa mbinguni mwema wapekee, mwana wake baba.


Mwenye kuondoa makosa ye-tu, utuhurumie maombi pokea.


Ku-u-me kwa Baba unapoketi, mtakatifu mku-u utuhurumie.


Pamoja na Roho M-takatifu, ndani yake Baba we’ unatukuzwa.


NASADIKI

Nasadiki Kwa Mungu mmoja

Baba mwenyezi muumba wa mbingu na nchi na vitu vyote,

(Vinavyoonekana na visivyo, na visivyoonekana) x 2


Mungu Baba ni muumba wa vyote, Yesu Kristu ni Mwana wa pekee, Maria ni mama yake kweli, aliteswa akafa sadaka.


Kafufuka siku ya tatu, alipaa huko uwinguni, Atarudi siku ya mwisho, ‘falmewake hauna mwisho.


Naye Roho ni mleta uzima, atokaye kwa Baba na Mwana, Huabudiwa pamoja naye, hunena Kwa vinywa vya manabii


Nasadiki kwa Kanisa moja, takatifu pia la kitume, Naungama ubatizo mmoja, nangojea u-zima wa milele.



MTAKATIFU

Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu Bwana Mungu wa majeshi x 2

Mbingu na dunia (mbingu) zimejaa utukufu wako x2


Hosanna, hosanna (hosanna) juu mbinguni x2


Mbarikiwa anayekuja kwa jina lake Bwana x 2



BABA YETU

Baba yetu uliye mbinguni (Baba) jina lako litukuzwe po-te, ufalme wako utufikie (Baba) utakalo Baba lifanyike x 2


Baba yetu mwema uliye mbinguni, jina lako Baba litukuzwe.


Na u-falme wako uje hapa kwetu, na mapenzi yako yatimizwe.


Tupe leo m-kate wa kila siku, utupe leo m-kate wetu.


Baba u-tusamehe makosa yetu, kama tusamehavyo we-nzetu.


Baba usituache vishawishini, ila utukinge na ma-ovu.


U-falme na nguvu nao utukufu, vyote ni vyako hata milele



MWANAKONDOO

Ewe Mwanakondoo wa Mungu

Unayeondoa dhambi zetu utuhurumie (mwanakondoo) utuhurumie x 2

Ewe Mwanakondoo wa Mungu

Unayeondoa dhambi zetu utuhurumie (mwanakondoo) utuhurumie x 2

Ewe Mwanakondoo wa Mungu

Unayeondoa dhambi zetu, utupe amani (Bwana) utupe amani, (Bwana) Utupe amani x 2

61 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page