top of page

BWANA UTUHURUMIE


Bwana Bwana (Bwana) tuhurumie

Bwana Bwana tuhurumie x 2

Kristu Kristu Kristu (tuhurumie)

Kristu Kristu tuhurumie x 2

Bwana Bwana (Bwana) tuhurumie

Bwana Bwana tuhurumie x 2


UTUKUFU


Sop: U-tukufu kwa Mungu juu

KIITIKIO:Na amani duniani (duniani), kwa watu wenye mapenzi mema x 2 (Amani)

1. Tunakusifu, tunakuheshimu, tunakuabudu, twakutukuza

2. Tunakushukuru Mfalme wa mbingu, Mwana wa pekee, Mwana wa Baba.

3 .Unayeondoa makosa yetu, utuhurumie tusikilize.

4. Kuume kwa Baba, unapoketi Mtakatifu mkuu tuhurumie.

5. Roho Mtakatifu, pamoja naye ndani yake Baba, unatukuzwa



NASADIKI


KIITIKIO:Nasadiki (mimi) ninasadiki, nasadiki (mimi) ninasadiki x 2 (kweli)

1. Nasadiki kwa Mungu Baba muumba wa vyote,

Nasadiki kwa Yesu Kristu mwana wa pekee,

Kwa uwezo wa roho Mungu katwaa mwili,

Na hapo Bikira Maria akawa Mamaye.


2. Kwa amri ya Ponsyo Pilato kasulubiwa,

Akafa na akazikwa kashuka kuzimu,

Siku ya tatu kafufuka, kapaa mbinguni,

Kaketi kuume kwa Baba, Kwa Baba mwenyezi.

3. Atarudi siku ya mwisho kutuhukumu,

Nasadiki kwa Roho Mfari-ji Mtakatifu,

Kanisa pia takatifu la Katoliki,

Ushirika wa wataka –tifu wa mbinguni.

4. Na maondoleo ya dhambi kwa ubatizo,

Ufufuko nao uzima ule wa milele x 2



MTAKATIFU


Mtakatifu/Mtakatifu Mtakatifu Mungu wa majeshi, mbingu na nchi / Mbingu na nchi zimejaa utukufu wako

Hossana juu x 3 Hossana Mbinguni x 2

(S/A) Mbarikiwa (yeye) mwenye kuja kwa jina la Bwana.



BABA YETU


KIITIKIO: Baba yetu wa mbinguni jina lako (Baba) litukuzwe

(Ufalme wako utufikie duniani kama mbinguni x 2)

Ufalme wako utufikie, duniani na kama mbinguni.

Utupe leo mkate wetu, utusamehe makosa yetu.

Usitutie kishawishini, utuopoe na maovu.

Ufalme nguvu na utukufu, vyote ni vyako hata milele.



MWANAKONDOO


Mwanakondoo, Mwana wa Mungu, unayeondoa makosa yetu (Mwana) tuhurumie x 2


S/A: Mwanakondoo wa Mungu, unayendoa makosa yetu.


Wote: Utujalie amani, utujalie (Mwana) utujalie amani x 2


10 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page