top of page


BWANA UTUHURUMIE

Bwana, Bwana tuhurumie,

Bwana, Ee Bwana tuhurumie x 2 sisi sote tuwakosefu.

Bwana, Ee Bwana tuhurumie.

Kristu, Kristu tuhurumie …………………………

Bwana, Ee Bwana tuhurumie……………………


UTUKUFU

Utukufu kwa Mungu juu na amani duniani Kwa watu wenye mapenzi, wenye mapenzi mema x 2

1. Twakusifu Bwana, twakuheshimu, twakuabudu na pia tunakutukuza.

2. Tunakushukuru, Mfal-me wa mbingu, Mwana wa peke-e pia Mwana wake Baba.

3. Mwenye Ku-ondoa dhambi za dunia, utuhurumie pia utusikilize

4. Uketiye ku-ume kwake Mungu Ba-ba, Mtakatifu mku-u utuhurumie.

5. Pamoja na Roho, Roho Mta-katifu, ndani yake Baba wewe unatuku-zwa.


BABA YETU

Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe, ufalme wako ufike, utakalo Baba lifanyike.

1. Tupe le-o Baba m-kate wetu, m-kate wetu wa kila siku.

2. Baba tusamehe makosa yetu, kama tusamehavyo we-nzetu.

3. Baba ‘situtie majaribuni, I-Ia utukinge na maovu.

4. Ufalme na nguvu na u-tukufu, vyote ni vyako hata milele.



MTAKATIFU

Sop: Mtakatifu Bwana (Mtakatifu Bwana) x 2 Bwana Mungu

Bwana Mungu wa majeshi x 2

Mbingu na dunia, (mbingu na dunia) x 2

Zimejaa zimejaa sifa zako x 2

Sop: Hosana x 2 Hosana juu mbinguni x 2

Mbarikiwa yule (mbarikiwa yule) x 2

Mwenye kuja kwa jina lake Bwana x 2


AMANI

Amani ya Bwana Yesu isambae kote, amani ya Bwana Yesu iwe nasi sote x2

Upendo…………...

Faraja…………………….. “ “ “ “ “ “

Furaha…………………….. “ “ “ “ “


MWANAKONDOO

Mwanakondoo wa Mungu uondoaye, dhambi za dunia, utuhurumie x 2

Mwanakondoo wa Mungu uondoaye, dhambi za dunia utupe amani,

Bwana utupe amani x 2


13 views0 comments

Comentários

Avaliado com 0 de 5 estrelas.
Ainda sem avaliações

Adicione uma avaliação
bottom of page