top of page

St. Joseph Mass


BWANA UTUHURUMIE


Sop: Bwana utuhurumie

Wote: Ee Bwana (T/B: Ee Bwana),

Wote: Sis tuwakosefu Bwana, twakuomba utuhurumie x 2

Kristu ‘tuhurumie kwani sisi tuwakosefu (A/T/B: Kristu, Kristu) All: Ewe Kristu utuhurumie x 2


UTUKUFU

Utukufu kwa Mungu juu na amani, kwa watu wenye mapenzi mema.

S/A: Tunakusifu, tunakuheshimu, tunakuabudu pia tunakutukuza

T/B: S-i-f-a na heshima ibada twakupa pia tunakutukuza

Alto: Tunakushukuru kwa ajili ya utukufu wako mkuu, ee Bwana Mungu mfalme wa mbinguni Mungu Baba Mwenyezi.

Sop: Ee Bwana Yesu Kristu Mwana wa pekee, Ee Bwana Mungu wa pekee, Ee Bwana Mungu Mwana Kondoo wa Mungu Mwana wa Baba.

Tenor: Mwenye kuondoa dhambi za dunia utuhurumie, ewe mwenye kuondoa dhambi za dunia pokea ombi letu, ewe mwenye kuketi kuume kwa Baba utuhurumie, utuhurumie.

Kwa kuwa ndiwe uliye peke yako Mtakatifu, peke yako Bwana peke yako mkuu Yesu Kristu, pamoja na Roho Mtakatifu katika utukufu wa Mungu Baba, Amina.



NASADIKI


Sop: Nasadiki kwa Mungu mmoja Baba mwenyezi mumba mbingu na nchi

Wote: Na vitu vyote vinavyoonekana na visivyo-onekana

Alto : Nasadiki kwa Bwana mmoja Yesu Kristu Mwana wa pekee wa Mungu.

Tenor: Aliyezaliwa kwa Baba tangu milele yote

All: Mungu aliyetoka kwa Mungu, mwanga kwa mwanga, Mungu kweli kwa Mungu kweli.

T/B: Aliyezaliwa bila kuumbwa, mwenye umungu mmoja na Baba ambaye vitu vyote vimeumbwa naye.

All: Ameshuka toka mbinguni kwa ajili yetu sisi wanadamu na kwa ajili ya wokovu wetu.

S/A : akapata mwili kwa uwezo wa Roho Mtakatifu,

All: kwake yeye Bikira Maria akawa mwanadamu.

S/A: Akasulibiwa pia kwa ajili yetu sisi akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato akafa akazikwa.

Wote: Akafufuka siku ya tatu ilivyoandikwa, akapaa mbinguni ameketi kuume kwake Baba, atakuja tena kwa utukufu

kuwahukumu wazima na wafu nao ufalme wake hautakuwa na mwisho.

S/A: Nasadiki kwa Roho Mtakatifu,

All Bwana mleta uzima

S/A Atokaye kwa Baba na mwana,

All Anayeabudiwa na kutukuzwa

A/T Pamoja na Baba na mwana,

All Aliyenenwa kwa vinywa na manabii.

T/B: Nasadiki kwa Kanisa moja,

All Takatifu Katoliki la mitume, naungama ubatizo mmoja kwa maondoleo ya dhambi, nangojea na ufufuko wa wafu na

uzima wa milele ijayo Amina.



FUMBO LA IMANI

Kristu alikufa, Kristu alifufuka, Kristu atakuja tena.


BABA YETU

Baba yetu wa mbinguni, Jina lako Baba litukuzwe, ufalme wako ufike (na) utakalo pia lifanyike x 2

1. Baba yetu uliye mbinguni jinalo litukuzwa, ufalme wako ufike, utakalo lifanyike, duniani kama mbinguni.

2. Utupe leo mkate wetu wa kila siku, utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe waliotukosea na sisi.

3. Usitutie kishawishini, lakini utuopoe maovuni x 2

4. Kwa kuwa ufalme ni wako, nguvu na utukufu hata milele.



MWANAKONDOO

Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia utuhurumie x 2

Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia utujalie amani, utujalie amani, utujalie amani x 2

Utujalie, utujalie (amani) utujalie amani.


3 views0 comments

Commenti

Valutazione 0 stelle su 5.
Non ci sono ancora valutazioni

Aggiungi una valutazione
bottom of page