top of page

St. Francis Mass


UTUHURUMIE

Bwana Bwana utuhurumie,

Sisi Bwana utuhurumie Ewe Bwana x 2

Kristu, Kristu tuhurumie Kristu tuhurumie,

Kristu, Kristu, Kristu, Kristu, Kristu tuhurumie,

Ewe Kristu, Kristu, Kristu, Kristu utuhurumie,

Kristu, Kristu, Kristu, Kristu Kristu, Kristu, Kristu.

Kristu, Kristu, Kristu tuhurumie.

Bwana Bwana utuhurumie

Sisi Bwana utuhurumie Ewe Bwana x 2


UTUKUFU

Utukufu kwa Mungu mbinguni na amani kote duniani, kwa watu wenye mapenzi mema (tena) kwa watu wenye, mapenzi mema.

1. Twakusifu kwa utukufu wako twakuheshimu tunakutukuza,

Ewe Mungu mfalme wa mbinguni ni wewe Mungu Baba mwenyezi.

2. Bwana Yesu Mwanaye wa pekee, Bwana Mungu Mwana wake

Baba, uondoaye dhambi za dunia, Bwana Yesu utuhurumie.

3. Uondoaye dhambi za dunia, Yesu Kristu pokea ombi letu,

Mwenye kuketi kuume kwa Baba, ni wetu Mwokozi utuhurumie.

4. Peke yako ndiwe Mtakatifu, peke yako mkuu Yesu Kristu,

Pamoja na Roho Mtakatifu, kwa utukufu wake Mungu Baba.


NASADIKI

Nasdiki kwa Mungu Baba Mwenyezi (ndiye) Muumba mbingu na nchi na vitu vyote (pia) (Nasadiki kwa Yesu Kristu mwanaye) x 2

1. Alitungwa kwa uwezo wa Roho kazaliwa na Bikira Maria,

Aliteswa kwa Pilato ‘a’kasulubiwa ‘a’kafa ‘a’kazikwa akashukia kuzimu.

2. Siku tatu kafufuka kapaa mbinguni kaketi kuume kwa Baba Mwenye enzi,

Toka huko atakuja kuwa hukumu wale wazima na wale wafu.

3. Kwake Roho Mtakatifu ninasadiki kanisa la katoliki la mitume,

ushirika wa watakatifu wa Mungu maondoleo ya dhambi nasadiki.

4. Nangojea ufufuko wa miili na uzima wa milele ijayo,

Nangojea ufufko wamiili na uzima wa milele amina.


MTAKATIFU

Mtakatifu Mungu wa majeshi

Mtakatifu, Mtakatifu Mungi wa majeshi

(Bass: Mbingu na dunia) Zimejaa zimejaa aa zimejaa utukufu wako mkuu

Hosanna (juu mbinguni) Hossana (juu mbinguni)

Hossana hosanna juu mbinguni.

Mbarikiwa anaye kuja kwa jina lake Bwana

Hossana (juu mbinguni) Hossana (juu mbinguni)

Hossana hosanna juu mbinguni.


FUMBO

(Huu ndio)

Mwili wa Bwana tusujudu tuabudu daima

(Hii ndio)

Damu ya Bwana tusujudu tuabudu daima


AMANI

(Tutakiane amani ya Bwana)

Tutakiane amani yake Bwana X 2

(Amani) amani yake Bwana (isambaee amani isambae

(Duniani) isambae daima milele

(Upendo)


MWANAKONDOO

Mwanakondoo wa Mungu unaye ondoa dhambi (za dunia)

Utuhurumie (Mwana) utuhurumie x 2

Mwanakondoo wa Mungu unaye ondoa dhambi

Utujali amani (Mwana) utujalie amani (Mwana)

Utujalie amani (Mwana) utujalie amani


BABA YETU

KIITIKIO: Baba yetu uliye mbinguni (jina) jina lako Baba litukuzwe

1. Duniani kama mbinguni (Baba) -utakalo lifanyike

tupe leo rziki zetu

2. Tusamehe makosa yetu - “

kama tunavyo wenzetu

3. Situtie kishawishini - “

Maovuni utuopoe

4. Kwa kuwa ufalme ni wako - “

Nguvu utukufu milele - “



BABA YETU

KIITIKIO: (Sop/Alto)-: Baba yetu uliye juu mbinguni, jina lako Baba, litukuzwe

Ufalme wako utufikie utakalo nalifanyike x 2

1. Duniani kama mbinguni tupe leo mkate wetu, mkate wetu wa kila siku ee Baba,

litukuzwe utakalo Baba Mungu nalifanyike.


2. Tusamehe makosa yetu kama tunavyosamehe, wale walio tukosea sisi ee Bwana

3. Situtie majaribuni walakini tuopoe maovuni ,ee Baba tuopoe ee Baba


4. Kwa kuwa ufalme ni waako na nguvu nao utukufu, Utukufu hata milele ee Bwana

0 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page